Home Local General Ajali ya Meli Mv Seagul zanzibar

Ajali ya Meli Mv Seagul zanzibar

Meli ya Seagul kabla ya kuondoka Dar es salaamMeli ya abiria ya STAR GIC mali ya kampuni ya SEAGUL iliyokuwa inasafiri kutoka DSM kwenda UNGUJA imezama katika bahari ya HINDI karibu na UNGUJA ikiwa na watu zaidi ya Mia Mbili themanini wakiwemo abiria Mia Mbili Themanini na Moja, watoto 31 na wafanyakazi Sita.

Mkurugenzi wa Utawala Shirika  la Bandari  Zanzibar Hamza Mohamedd Ali amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo tayari baadhi ya maiti wamefikishwa katika bandari ya ZANZIBAR huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Hapa DSM mwandishi wetu RAMADHAN MPENDA aliweza kufika katika bandari ya DSM ambapo alishuhudia jamaa na ndugu wakisubiri hatma ya ndugu zao waliokuwa wakisafiri na meli hiyo ya STAR GIC mali ya kampuni ya SEAGUL bila kufahamu la kufanya kutokana na maelezo kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikiendesha shughuil zake bila kuwa na ofisi rasmi.

Baadhi ya abiria watu waliokuwepo bandari wamedai kuwa wamekuwa wakikatia tiketi katika maeneo yasiyo rasmi.

Kufuatia taarifa za kutokea kwa ajali hiyo, huko bungeni mjini DODOMA kikao cha bunge kimeahirishwa hadi kesho saa TAtu asubuhi baada ya aziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. EMMANUEL NCHIMBI kuomba kuondolewa kwa hoja iliyokuwa ikiendelea ya kuhitimisha bajeti yake na badala yake kushughulikia suala linguine muhimu.

Spika ANNE MAKINDA alikubali hoja hiyo na baada ya kuhoji bunge lilikubali kufanya  hivyo na kuahirisha kikao.

 

Last Updated ( Thursday, 19 July 2012 02:11 )  
Banner