Home Local General Serikali yafafanua bomoabomoa maeneo ya hifadhi

Serikali yafafanua bomoabomoa maeneo ya hifadhi

Waziri wanchi ofisi ya makamu wa Rais – mazingira, Terezya Huviza Serikali imetoa ufafanuzi juu baraza la Taifa la usimamizi na hifadhi ya mazingira – NEMC kuendesha bomoa bomoa kando ya mito na fukwe za bahari.

Maeneo yaliyokumbwa na nyumba 17 na uzio wa nyumba nane kubomolewa ni kando ya mito na fukwe za bahari za  Mbezi, Mawe, Mndumbwe na maeneo ya hifadhi ya mikoko.

Tamko hilo limetolewa mjini Dodoma na waziri wanchi ofisi ya makamu wa Rais – mazingira Terezya Huviza mbele ya waandishi wa habari kufuatia kuwepo kwa baadhi ya watu kutoa malalamiko na wengine kukimbilia mahakamani kuomba zuio la kutokubomolewa nyumba zao.

Tamko hilo limekuja huku kukiwa pia na vitisho mbali mbali vinavyotolewa na watu wasiofahamika vikielekezwa kwa viongozi wa baraza la taifa la usimamizi wa  mazingira NEMC na kwa waziri Huviza mwenyewe.

Tamko hilo pia linawataka wale waliovunjiwa nyumba zao katika awamu ya kwanza kulipa gharama zote za zoezi hilo ambazo ni shilingi milioni hamsini.

Rahel Muhando, TBC Dodoma.

Last Updated ( Wednesday, 18 July 2012 03:24 )  
Banner