Home Local General TANESCO yabaini inavyohujumiwa na baadhi ya wateja

TANESCO yabaini inavyohujumiwa na baadhi ya wateja

Meneja wa kituo cha  TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (ki-TANESCO), Christopher MasasiOperesheni inayofanywa na shirika la umeme nchini TANESCO kubaini watu wanaojiunganishia umeme kinyume cha sheria imeendelea ambapo katika baadhi ya maeneo mafundi wa shirika hilo wamebaini wateja waliochakachua mita za umeme na kusababishia shirika hasara.

Katika maeneo ya Kinondoni, mafundi wa TANESCO wameshuhudia baadhi ya wateja wakiwa wamejihusisha na vitendo vya kuliibia shirika hilo umeme kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mita za luku, kujenga laini za umeme isivyo halali pamoja na kuunganisha umeme moja kwa moja kutoka kwenye nguzo za umeme ambapo taarifa za hivi karibuni zinasema katika mita 114 zilizokaguliwa, mita 19 zimechakachuliwa.

Meneja wa Kituo cha  TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (ki-TANESCO) Christopher Masasi, ametoa mbinu  kwa  wafanyakazi wa shirika hilo na kupanga mikakati ya utekelezaji wa kazi ya  kuwabaini wateja wa shirika hilo waliojiunganishia umeme isivyohalali katika eneo lake.

Utekelezaji wa zoezi hilo ulianzia eneo la  Morocco Manispaa ya Kinondoni na mafundi wa shirika hilo kubaini mita zilizofunguliwa lakiri  katika baadhi ya nyumba na kuharibiwa uwezo wake  wa kusoma gharama halisi za umeme.

Operesheni kama hiyo imefanyika pia katika Mkoa wa Ki-TANESCO, Temeke na Ilala ambapo Meneja wa Ilala Injinia Athanaus Nangali ameelezea changamoto za operesheni katika Mkoa wake.

Aaron Mrikaria, TBC Dar es Salaam.

Last Updated ( Wednesday, 18 July 2012 03:19 )  
Banner