Home Local General Mkutano uvuvi na biashara wafanyika Dar

Mkutano uvuvi na biashara wafanyika Dar

Mkuu wa kitengo cha Uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni makamu mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Adolf Mkenda Wajumbe zaidi ya 300 kutoka nchi mbalimbali duniani wanataraji kushiriki katika mkutano wa kimataifa wa uchumi wa uvuvi na biashara utakaonza kesho jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa 16 unaofanyika kwa mara ya kwanza nchini na katika nchi zilizo ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara unataraji kuona ripoti mia moja za kitafiti zinazohusiana na uvuvi kutoka mabara ya Afrika, Ulaya, Amerika na Asia zikiwasilishwa.

Fursa za kiuchumi zilizopo katika uvuvi na ufugaji wa samaki pamoja na mazao ya vyakula vitokanavyo na bahari, hii ndo kauli mbiu ya mkutano wa 16 wa kimataifa wa uvuvi wa kiuchumi na biashara utakaofanyika jijini Dar es Salaam kwa uratibu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye ni makamu mwenyekiti wa mkutano huo, Dkt. Adolf Mkenda amesema mkutano huo wenye lengo la kulinda na kutoa fursa za kiuchumi kwa viumbe vya baharini utaleta tija katika sekta ya uvuvi nchini.

Dkt. Mkenda amesema teknolojia katika uvuvi imekuwa ni kikwazo cha kuvua katika maji marefu na kusema mkutano huo utasaidia kuleta changamoto kwa taifa ya jinsi gani ya kuboresha uvuvi ili uweze kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa.

Grace Kingalame, TBC Dar es Salaam.

Last Updated ( Wednesday, 18 July 2012 03:12 )  
Banner