Home Local General Mulongo akemea wanaopinga Sensa

Mulongo akemea wanaopinga Sensa

 Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua watu wanaoshawishi migogoro katika kufanikisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwani hilo jambo ni jambo ambalo limepangwa kitaifa.

Amesema tayari serikali ilishatoa maagizo mbali mbali kwa jamii kinachotakiwa ni wananchi kufuata taratibu zote ili waweze kuhesabiwa kwa wakati muafaka na si kudanganywa na vikundi vya watu wachache.

Mulongo ametoa wito kwa wananchi kufuatia baadhi ya watu kuibuka na kutoa vishawishi vya kutaka kuwarubuni watu wasijitokeze katika zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 26, ambapo tayari maandalizi yameanza ikiwemo wakufunzi 158 ambao wanakutana Jijini Arusha kupata mafunzo ya siku 12 ya namna yakufanikisha zoezi la sensa.

Kufuatia changamoto hiyo,Mkuu wa mkoa amewaagiza wakufunzi hao kutumia uzalendo katika kuhakikisha wanafanikisha zoezi la sensa Agosti 26.

Sechelela Kongola, TBC Arusha.

Last Updated ( Wednesday, 18 July 2012 03:15 )  
Banner