Home Local General Kituo cha kulelea watoto chapungukiwa watoto

Kituo cha kulelea watoto chapungukiwa watoto

Sister Mary Clesencia Mulla  Kituo cha kulelea watoto yatima cha Antonio Rosemin kilichopo kijiji cha Kwediboma wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kinakabiliwa na tatizo la uhaba wa watoto wa kulea kutokana na hofu pamoja na uelewa mdogo walionao wakazi wa kijiji hicho.

Sister Mary Clesencia Mulla  amesema hofu ya kuchukuliwa watoto kupelekwa nje ya nchi, kubadilishwa dini na kukatwa viungo vyao ndio inayowafanya wanakijiji kukataa kuwapeleka yatima kituoni hapo.

Kituo hicho kinauwezo wa kuwahudumia watoto ishirini lakini mpaka sasa wapo tisa tu.

Mwenge wa uhuru umefika kijijini hapo kutembelea watoto hao na kiongozi wa mbio za mwenge Kapteni Honesti Mwanossa akawahamasisha wananchi juu ya matumizi ya kituo hicho.

Kituo hicho kimeamua kuchukua watoto kuanzia umri sifuri hadi miaka mitano kwakuwa  ndio wanaoshambuliwa sana na maradhi, lengo likiwa ni kuwapa uangalizi  mzuri na kuhakikisha wanakuwa wakiwa na afya njema.

Fatma Matulanga, TBC Kilindi-Tanga.

Last Updated ( Friday, 13 July 2012 15:31 )  
Banner