Home Local General Ahamadia wahamasisha ushiriki Sense

Ahamadia wahamasisha ushiriki Sense

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadia nchini, Abraham AhmedKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadia nchini Abraham Ahmed amewataka waislamu na watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi ili kuwezesha kupatikana kwa takwimu sahihi zitakazoiwezesha serikali kupanga mipango endelevu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Katibu mkuu huyo wa Ahmadia amesema zoezi la sensa ya watu na makazi lina manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa na watu wake na kuwataka waislamu kuwapuuza wale wote wanaobeza zoezi hilo sanjari na kuendelea kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Amicus Butunga, TBC Mwanza.

Last Updated ( Friday, 13 July 2012 15:29 )  
Banner