Home Local General CCM Tabora yaonya maDC, Wanahabari kutojihusisha na mchakato wa chaguzi

CCM Tabora yaonya maDC, Wanahabari kutojihusisha na mchakato wa chaguzi

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora, Hassan Mwakasuvi Chama cha Mapinduzi mkoani Tabora kimewaonya Wakuu wa Wilaya za mkoa huo kutojihusisha hata kidogo katika mchakato wa kuwapata viongozi mbali mbali wa Chama hicho wanaogombea kwenye maeneo yao.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassan Mwakasuvi katika Kongamano la Wanahabari lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari ya mkoa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Suleiman Kumchaya Naye mkuu wa Wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akawakumbusha Wanahabari kufanyakazi zao kwa kuzingatia miiko ya kazi na kuwaonya watu wanaovamia kazi hiyo bila kuwa na Taaluma.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatuma Mwassa Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa amesema vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa, hivyo ametoa wito kwa wadau hao kuvitumia katika shughuli za maendeleo ya mkoa. 

Mratibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Tabora Job Chimwaga amesema klabu hiyo ipo tayari kushirikiana na mkoa katika kuendesha jarida la mkoa pindi litakapoanza.

Nico Mwaibale, TBC Tabora.

Last Updated ( Wednesday, 11 July 2012 11:31 )  
Banner