Home Local General Polisi kuchunguza tuhuma za viongozi CHADEMA kutakiwa kuuawa

Polisi kuchunguza tuhuma za viongozi CHADEMA kutakiwa kuuawa

Waziri wa mambo ya ndani, Dr. Emmanuel NchimbiWaziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi ametoa tamko la serikali kuhusu tuhuma zilizonukuliwa na vyombo vya habarí nchini za viongozi wa chama cha CHADEMA kutakiwa kuuawa wanazodai kuratibiwa na taasisi ya vyombo vya dola nchini.

Katika tamko hilo lililotolewa na waziri nchimbi mjini Dodoma mbele ya waandishi wa habarí, amesema kuwa tuhuma hizo ni nzito ambazo serikali haiwezi kuzifumbia macho.

Dr. Nchimbi amesema pamoja na kwamba viongozi wa CHADEMA wamekataa kutoa taarifa hizo kwa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi, yeye kama waziri mwenye dhamana ameliagiza jeshi hilo kuwahoji walioibua tuhuma hizo.

Hata hivyo waziri Nchimbi amesema  serikali haitasubiri wala haiombi kutekeleza wajibu wa kulinda raia.

Last Updated ( Tuesday, 10 July 2012 12:47 )  
Banner