Home Local General CCM Misungwi yamtaka Mwenyekiti wa halmashauri kujiuzulu

CCM Misungwi yamtaka Mwenyekiti wa halmashauri kujiuzulu

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Benard Polycarp Kamati ya siasa ya chama chamapinduzi (CCM) wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza imempa siku tatu kuanzia julai tisa mwaka huu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Benard Polycarp kujiuzulu wadhifa wake kwa kutumia vibaya madaraka yake na kuruhusu kufanyika kwa ubadhirifu huo.

Hali hiyo inatokana na sakata la ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini mwanza, katibu wa CCM wilaya ya Misungwi Marco Kahuruda ameonya kuwa baada ya muda huo kumalizika ifikapo julai 11 mwaka huu, mwenyekiti huyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama hicho ikiwemo kuvuliwa uanachama.

Wajumbe wa kamati ya siasa ya chama chamapinduzi (CCM) wilaya ya Misungwi Siku chache baada ya kamati ya siasa ya chama chamapinduzi(CCM) mkoani Mwanza kuiagiza kamati ya siasa ya chama hicho katika wilaya ya misungwi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini na kuwachukulia hatua madiwani wa CCM wanaotuhumiwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kufuja mabilioni ya fedha za umma, uongozi wa CCM wilaya ya misungwi umekutana na waandishi wa habari na kubainisha matokeo ya uchunguzi huo ambapo imebainika kuwa kuna ushiriki wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Benard Polycarp katika ubadhirifu wa fedha za umma.

Kwa upande wake mwenyekiti huyo wa halmashauri ya wilaya ya misungwi hakuwa tayari kuzungumzia namna alivyopokea maagizo hayo ya kamati ya siasa.

Wakati hayo yakijiri wilayani Misungwi, halmashauri kuu ya CCM mkoani Mwanza imekutana jijini Mwanza na kuzungumzia masuala kadhaa likiwemo zoezi la ununuzi wa pamba.

TBC Mwanza.

Last Updated ( Tuesday, 10 July 2012 12:43 )  
Banner