Home Local General Teknolojia ya kilimo funika yaanza kutumika Morogoro

Teknolojia ya kilimo funika yaanza kutumika Morogoro

Afisa Kilimo na Mifugo tarafa ya mikese, Anna Basili  Teknolojia ya kilimo cha mazao -funika imeanza kutumia katika vijiji vinne vya kata ya mkambarani wilaya ya morogoro vijijini , lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao  katika maeneo yenye ukame.

Wagani wa kilimo katika vijiji na kata hiyo kwa kushirikiana na watafiti wa kilimo wamedhamiria kusambaza teknolojia hiyo pia ili kudhibiti magugu angamizi ya mazao yajulikanayo kama strigers au kiduha ambayo husambaza mbegu zake ardhini takribani 20,000 kwa gugu moja zenye uwezo wa kuhimili ardhini kwa miaka 50 huku zikiangamiza mazao.

Kilimo cha mazao – funika ambacho kinachanganywa na mazao ya mikunde aina ya fiwi na magobe kimeonyesha mafanikio katika tafiti za maeneo yenye ukame katika vijiji vya mkambarani wilaya ya Morogoro eneo ambalo lilikuwa halizalishi zao lolote kutokana na ukame na pia kuwepo kwa magugu ya kiduha lakini baada ya majaribio hayo eneo hilo lenye ukubwa wa robo ekari limeweza kuzalisha gunia angalau mbili.

Afisa utafiti kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Mlingano Atanasio Malandu, Afisa Kilimo na Mifugo tarafa ya mikese Anna Basili  na afisa kilimo na mifugo kata ya mkambarani Leah Luwasa kwa pamoja wmefafanua kuwa kilimo hicho kitakuwa ni mkombozi kwa wakulima.

Nao wanakikundi wa kilimo kwanza Ramadhani Kidukuli na Ahmed Tembo wamesema lengo lao ni kusambaza kilimo hicho kwa wakulima wa vijiji vine vya Mkambarani, Kizinga, Mkono wa Mara na Pangawe kupitia shamba darasa.

Praxeda Mtani, TBC Morogoro .

Last Updated ( Thursday, 07 June 2012 12:16 )  
Banner