Home Local General Rais Kikwete ahitimisha kilele cha siku ya mazingira

Rais Kikwete ahitimisha kilele cha siku ya mazingira

Rais Jakaya Kikwete Rais Jakaya Kikwete amehitimisha kilele cha siku ya Mazingira duniani Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kukiri kuwa hali ya uharibifu mazingira ni mbaya na kwamba jitihada zisipochukuliwa nchi itakuwa gizani kutokana na vyanzo vya maji kukauka.

Rais Kikwete amesema asilimia kubwa ya uharibifu huo umesababishwa na shughuli za kibinadamu hali ambayo maeneo mengi yamekuwa  jangwa.

JK akizindua kampeni ya taifa usafi wa mazingira

Rais Kikwete amehitimisha kilele cha siku ya Mazingira duniani kilichofanyika katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo ameshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la wazi la Uhuru hotel.

Katika shughuli hiyo, Rais Kikwete pia amezindua kampeni ya Kitaifa ya usafi wa mazingira ambapo naibu waziri wa afya Dokta Seif Rashid amesema hali ya usafi wa mazingira nchini hairidhishi hivyo kila mtu anatakiwa kufanya usafi pamoja na kujenga vyoo ili kuhakikisha nchi inapiga hatua ya kufikia malengo ya milenia.

Sauda Shimbo, TBC Moshi.

Last Updated ( Wednesday, 06 June 2012 10:53 )  
Banner