Home Local General Ziwwa achaguliwa uspika Bunge la Afrika Mashariki

Ziwwa achaguliwa uspika Bunge la Afrika Mashariki

Spika mpya wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki,Magreth Ziwwa kutoka UgandaWabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamepiga kura na kumchagua Magreth Ziwwa kutoka Uganda kuwa spika wa bunge hilo ambaye ataliongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Wabunge hao wamekutana jijini Arusha kwa mara ya kwanza nakufanya uchaguzi huo pamoja na wao wenyewe kula kiapo cha bunge mbele ya spika huyo.

Mara baada ya kupiga kura katibu mkuu wa bunge akatangaza matokeo ambapo Mgombea Magreth Ziwwa amepata kura 33 huku mpinzani wake Dora Dyamka akipata kura 12. 

Zoezi la kumchagua spika huyo wa bunge la Afrika Mashariki lililazimika kurudiwa mara mbili kufuatia wagombea kutopata theluthi mbili kwa mujimu wa mkataba wa bunge la jumuiya hiyo.

Sechelela Kongola/ Khalifa Mshana, TBC Arusha.

Last Updated ( Wednesday, 06 June 2012 10:49 )  
Banner