Home Local General Kamati ya bunge yataka uendeshaji KIA kuboreshwa

Kamati ya bunge yataka uendeshaji KIA kuboreshwa

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zainab Vullu Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali imetembelea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro- KIA na kusema kuwa wakati umefika kwa serikali kutoa maamuzi ya uwezekano wa kuendesha uwanja huo ambao unakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zainab Vullu wakati akitoa majumuisho ya ziara hiyo ambapo amesema kama serikali itashindwa kuendesha uwanja huo ni vyema kutafuta mwekezaji.

Mjumbe wa kamati hiyo, Ali Mohamed Kesi Ziara hiyo ya kamati ya bunge ya hesabu za serikali katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro imeiwezesha kamati hiyo kujionea changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa karakana ya kufanyia ukarabati ndege ambayo haijatumika tangu ilipojengwa mwaka 1980.

Mjumbe wa kamati hiyo, Ali Mohamed kesi amesema ni vyema serikali ikaangalia upya bodi iliyopo. Kamati hiyo pia imekutana na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro na kuuagiza kupitia upya mkataba wa mkandarasi anayejenga jengo jipya la chumba cha upasuaji cha Hospitali ya mkoa Mawenzi.

Sauda Shimbo, TBC Moshi.

Last Updated ( Wednesday, 06 June 2012 10:48 )  
Banner