Home Local General Kesi dhidi ya Askofu Hotay yaahirishwa

Kesi dhidi ya Askofu Hotay yaahirishwa

Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay Kesi inayomkabili Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay ambayo ilikuwa inatakiwa kutolewa maamuzi ya msimamo kuhusu kesi hiyo imeahirishwa baada ya Jaji wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatma Masengi kupata dharura.

Akiahirisha kesi hiyo Msajili wa mahakama kuu kanda ya Arusha, Georg Albart ameiambia mahaka kuwa kesi hiyo itatolewa uamuzi Agosti 15 mwaka huu kutokana na Jaji anayeisikiliza kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu.

Majira ya asubuhi katika mahaka kuu kanda ya Arusha ambapo hali ikiwa tulivu na watu wachache kukaa katika makundi wakisubiri kuanza kwa kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Anglikana Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay ili kufahamu iwapo kesi hiyo itasikilizwa au itatupiliwa mbali.

Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa mwaka jana na waumini watatu kwa ajili ya kupinga uchaguzi wa Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro kwa madai kuwa hajatimiza vigezo vya kuwa Askofu pamoja nakudai kuwa vyeti vyake vinaonyesha kugushi umri.

Wakati huo huo mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeshindwa kuanza kusikiliza kesi inayowakabili viongozi wa CHADEMA pamoja na wafuasi wake tisa baada ya wakili wa upande wa utetezi Method Kimomogoro kuwasilisha ombi, mahakama Kuu Kanda ya Arusha yakutaka kupitia kesi tatu tofauti zinazowakabili viongozi na wafuasi wa chama hicho.

Kufuatia hatua hiyo, Hakimu mkazi Charles Magesa amekubaliana na ombili la wakili huyo ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 4.

Sechelela Kongola, TBC Arusha.

Last Updated ( Wednesday, 06 June 2012 10:43 )  
Banner