Home Local General Baadhi ya wakazi wa Tarime waonyesha hofu kuhesabiwa

Baadhi ya wakazi wa Tarime waonyesha hofu kuhesabiwa

Mkuu wa mkoa wa Mara, John TuppaWakati juhudi za kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa likiendelea nchini, Imebainika kuwa baadhi ya wananchi wa wilayani Tarime wanaogopa zoezi hilo kwa madai kuwa kama watahesabiwa watakufa.

Kutokana na hofu hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa amewaondoa hofu wananchi hao na kusema kuwa sio kweli kama mwananchi akihesabiwa atakufa bali zoezi la sensa linalenga kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga, kutelekeza na kutathmini mipango mbalimbali ya maendeleo.

Hali hiyo ilibainishwa katika kikao maalum cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Mara cha kupitisha bajeti ya mwaka 2012/2013 ambapo pamoja na bajeti kujadiliwa kwa kina suala la sensa ya watu na makazi likaibuliwa kwa hofu kuwa baadhi ya wananchi hasa wilayani TARIME wanakabiliwa na uoga kuwa kama watahesabiwa basi safari ya kuishi duniani itakuwa imefikia tamati.

Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa amewaondoa hofu wananchi kuhusu zoezi hilo.

Suala lingine lilioibuliwa katika kikao hiki ni ujenzi wa barabara ya Makutano- Musoma hadi Mto wa Mbu Arusha kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake unasubiriwa kwa hamu na wananchi ili kuondoa adha wanayopata kwa sasa.

Emanuel Amas, TBC Mara.

Last Updated ( Wednesday, 16 May 2012 11:52 )  
Banner