Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home Local General Fedha za UKIMWI Ziwafikie Walengwa- Kandoro

Fedha za UKIMWI Ziwafikie Walengwa- Kandoro

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro Mkuu wa mkoa wa MBEYA ABBAS KANDORO amesikitishwa na taasisi, asasi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa yakipatiwa fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI lakini fedha hizo zinadaiwa haziwafikii walengwa.

KANDORO ametoa kauli yake wakati wa mkutano wa wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI ambao pamoja na mambo mengine wadau hao, wanafanya tathimini ya matumizi ya fedha zinazotolewa na wahisani kabla ya utekelezaji wa awamu ya tisa ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa dharula wa UKIMWI-RAPID FUND ENVELOP.

Serikali kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali kutoka nje ya nchi kupitia tume ya kudhibiti Ukimwi nchini-TACAIDS wamekuwa wakitenga mafungu kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi,tangu mwaka 2002

Tayari mfuko wa dharula umetoa zaidi ya bilioni 30 kama ruzuku kwa mashirika na asasi mbalimbali nchini.

Last Updated ( Friday, 27 January 2012 13:37 )  
Banner