Mkuu wa wilaya ya Kilwa NURDIN BABU amewataka madiwani, wenyeviti wa serikali na watendaji wa vijiji kusimamia vizuru suala la ardhi katika maeneo yao ili kuhakikisha akina mama wajane na wenye ulemavu hawadhulumiwi ardhi
BABU ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji kutoka kata tisa za wilaya ya Kilwa yaliyoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya LIWOPAC
Amesema migogoro mingi ya ardhi inayotokea wilayani humo inatokana na baadhi ya watendaji wa vijiji kutokaa na kuzungumzia suala hilo badala yake wanakuza migogoro na kuwa mikubwa.
Kwa upande wao wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wamelishukuru shirika la LIWOPAC kwani wananchi wengi wa vijijini wanadhurumiwa ardhi kwa kuwa hawajui sheria zao na sasa wamepata uelewa.
