Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home Local General Jaji Ramadhani Azungumza Kusimamishwa kazi kwa Nancy Baraza

Jaji Ramadhani Azungumza Kusimamishwa kazi kwa Nancy Baraza

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino RamadhaniJaji Mkuu Mstaafu, AUGUSTINO RAMADHANI amesema ni jambo la kawaida hasa katika nchi za jumuiya ya madola kuunda jopo maalum kuchunguza majaji wanaotuhumiwa kwenda kinyume na taratibu za kinidhamu.

Jaji RAMADHAN alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wa serikali ya KENYA kumsimamisha kazi na kisha kumchunguza Naibu Jaji Mkuu wa serikali ya nchi hiyo NANCY BARAZA ambaye anatuhumiwa kumtishia kwa bastola mmoja wa walinzi  jijini NAIROBI, mwishoni mwa mwaka jana.

Jaji RAMADHANI ni mmoja wa wajumbe saba wa jopo lililoteuliwa  na serikali ya KENYA kuchunguza  tuhuma zinazomkabili BARAZA.

Last Updated ( Friday, 27 January 2012 13:28 )  
Banner