Home Kenya Jordan yaandaa makambi kuhifadhi wakimbizi wa Syria

Jordan yaandaa makambi kuhifadhi wakimbizi wa Syria

JordanJordan imeandaa makambi maalumu kwaajili ya kuwahifadhi wakimbizi wa machafuko yanayoendelea nchini Syria, wanaokimbilia nchini humo kwaajili ya kupata hifadhi na mahitaji muhimu.

Hali ya mgogoro wa Syria uliodumu kwa kipindi cha miezi kumi na nane sasa haijapata suluhisho licha ya Umoja wa mataifa kuzitaka pande zinazopingana nchini humo  kumaliza mapigano kwa njia ya mazungumzo ili kuepuka kuendelea kupoteza maisha ya raia wasiokuwa na hatia nchini humo.

Katika hatua nyingine mjumbe maalumu wa umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria Koffi Annan yupo nchini Iran kujadili namna ya kutatua mgogoro wa Syria.

Katika mazungumzo hayo kuhusu kurejesha amani chini Syria, Annan atawahusisha viongozi wa serikali ya Syria pamoja na washirika wakubwa wa nchi hiyo.

Last Updated ( Wednesday, 11 July 2012 10:53 )  
Banner