Home Kenya UN yataka mapigano Syria kuamalizwa kwa mazungumzo

UN yataka mapigano Syria kuamalizwa kwa mazungumzo

Naibu mjumbe wa Umoja wa mataifa wa kutatua mgogoro wa mapigano Syria, Jean Marie Guehenno Umoja wa mataifa umezitaka pande zinazopingana nchini Syria kumaliza mapigano yanayoendelea nchini humo kwa njia ya mazungumzo ili kuepuka kuendelea kupoteza maisha ya raia wasiokuwa na hatia nchini humo.

Akizungumzia hatua hiyo, naibu mjumbe wa Umoja wa mataifa katika kutatua mgogoro wa mapigano nchini Syria Jean Marie Guehenno amesema pande zote zina wajibu wa kulinda maisha ya raia nchini humo ambao wamekuwa waathirika wakubwa katika mapigano yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Amesema umoja wa mataifa unaukubali mpango wa kufanya mabadiliko ya ungozi nchini Syria kwa kuzingatia njia za amani ili kufikia malengo yatakayokuwa na manufaa kwa wananchi wa Syria, ambapo amesema kumekuwa na hali ya mvutano baina ya Marekani na Russia juu ya utawala wa Rais Bashar Al Assad wa Syria, ambapo Russia inapinga pendekezo la Marekani la kutumia nguvu kuondoa utawala wa Rais Bashar Al Assad nchini humo.

Last Updated ( Friday, 06 July 2012 11:28 )  
Banner