Home Kenya Walionusurika kifo Syria wasimulia walivyovamiwa

Walionusurika kifo Syria wasimulia walivyovamiwa

SyriaBaadhi ya watu walionusurika kuuwawa katika mashambulio yanayoendelea nchini Syria wameeleza jinsi wauwaji walivyovamia nyumba zao na kuwauwa baadhi ya wanafamilia mauaji yakitokea katika mji wa Houla

Mjumbe wa amani nchini Syria, Kofi Annan

Baadhi ya mashuhuda hao wameelezea jinsi walivyopigwa huku wengine wakieleza namna walivyo jifanyisha kama wamekufa

Pamoja na wengi wa mashuhuda hao kudai kuwa wanajeshi na kundi linaloogopwa la Shabiha kuhusika katika mauaji hayo lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha na kusisitiza vitendo hivyo kufaywa na kundi la waasi.

Mjumbe wa amani nchini Syria, Kofi Annan amewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus kwa ajili ya mazungumzo na serikali juu ya mpango wa kuleta amani nchini humo.

 

Last Updated ( Tuesday, 29 May 2012 12:09 )  
Banner