Home Kenya Hukumu ya daktari wa Osama yapokewa kwa hisia tofauti

Hukumu ya daktari wa Osama yapokewa kwa hisia tofauti

Daktari wa Osama Bin Laden, Shakeel Afridi Watu mbalimbali duniani wamepokea kwa hisia tofauti hatua ya serikali ya Pakistan kumhukumu kifungo cha miaka 33 jela daktari maarufu nchini humo Shakeel Afridi baada ya kutiwa hatiani kwa uhaini.

Baadhi ya majirani wa daktari huyo nchini Pakistan wamesema adhabu aliyopewa ni ndogo kutokana na vitendo vyake vya kulisaliti taifa lake kwa maslahi ya serikali ya Marekani. Marekani nayo inasema haioni sababu za serikali ya Pakistan kumfunga Afridi kwa vile hana hatia.

Afridi anatuhumiwa kuwapatia taarifa maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani, CIA zilizosaidia kukamatwa na kuuawa kwa kiongozi wa kikundi cha kigaidi cha Al-Qaeda, Osama Bin Laden mjini Abbottabad nchini Pakistan alikokuwa akiishi na familia yake.

Serikali ya Pakistan imedai kuwa daktari huyo alijidai kufanya kampeni ya chanjo ya Polio nchini humo lakini badala yake alitumia kampeni hiyo kufanya uchunguzi na kujua mahali alipo Osama na kisha kutoa taarifa kwa CIA walioshambulia eneo hilo na kumuua.

Last Updated ( Thursday, 24 May 2012 12:17 )  
Banner