Mahakama kuu nchini Pakistan imesema itaangalia upya kinga ya kutoshitakiwa aliyowekewa rais wa nchi hiyo katika wiki mbili zijazo, itakapokuwa ikisiliza kesi ya kudharau amri ya mahakama inayomkabili waziri mkuu wa Pakistan Yusuf Raza Gillan.
Akijitetea mahakamani hapo Raza amesema kwa mujibu wa sheria za Pakistan rais wa nchi hiyo ana kinga ya kutoshitakiwa ndio maana alishindwa kumfungulia mashtaka ya ubadhirifu wa mali ya umma rais Gillan Asif Ali Zardari kama alivyoamriwa na mahakama kuu ya Pakistan.
Mwaka 2003 Zardari pamoja na mke wake hayati Benazil Bhuto walifunguliwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma na benki moja ya nchini Switzerland kuamua kushikilia zaidi ya dola Milioni sitini za Marekani walizokuwa wameziweka katika benki hiyo.
Hata hivyo mwaka 2007 walipata msamaha na fedha zao kuachiwa, ingawa mwaka 2008 serikali ya Pakistan iliyokuwa madarakani iliwafungulia tena mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma dhidi ya Zardari.
