Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home Kenya Uopoaji miili kwenye meli ya Costa Concordia kuendelea tena

Uopoaji miili kwenye meli ya Costa Concordia kuendelea tena

Meli ya Costa Concordia baada ya kuzamaWaokoaji nchini Italia wanatarajia kuanza tena kazi yenye changamoto ya kutafuta miili ya watu walionasa katika meli ya kifahari ya Costa Concordia iliyokwenda mrama na kisha kupinduka katika kisiwa cha Julio kilichoko kwenye visiwa vya Tasker ijumaa iliyopita.

Zoezi la kuopoa miili katika meli hiyo limesimamishwa mara kadhaa na kuanza tena kutokana na hali mbaya ya hewa. Hata hivyo waokoaji wanasema itabidi wafanye kazi hiyo kwa haraka sana wakihofia meli hiyo kudidimia katika vilindi vya bahari.

Wamesema watakwenda hadi katika ghorofa ya nne ya meli hiyo mahali ambako kulikuwa na mgahawa kwa vile miili ya watu kadhaa ilipatikana katika eneo hilo na wanamatumaini kupata miili zaidi katika eneo hilo. Bado watu 20 waliokuwa ndani ya meli hiyo hawajulikani walipo na inasemekana bado wamenasa ndani ya meli hiyo.

Majirani za za hodha wa meli ya Costa Concordia, Francesco Schettino aliyeko katika kizuizi cha nyumbani katika mji wa Meto Di Sorento wameendelea kumtetea jirani yao na kudai kuwa hana hatia. Wanasema vyombo vya habari ndio vinajaribu kumhukumu kwa kufanya habari yake kuwa kubwa, lakini wamesema wanampongeza kwa kazi nzuri.

Last Updated ( Thursday, 19 January 2012 15:53 )  
Banner