Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home Kenya

Kenya

Makanisa ya kiprotestanti yaanza mkutano Ujerumani

Makanisa ya kiprotestanti yaanza mkutano Ujerumani

Mkutano wa 34 wa Makanisa ya Kiprotestanti nchini Ujerumani, Kirchentag, umefunguliwa rasmi mjini Hamburg nchini humo, huku ukiwa umebeba agenda kadhaa ikiwemo kudorora kwa amani na tishio la ongezeko la matabaka kati ya matajiri na masikini duniani.

Mkutano huo wa siku tano, unaozishirikisha zaidi ya nchi 85 duniani kote wakiwemo wajumbe kutoka Tanzania, umelenga kujadili njia bora za kuhakikisha kuwa dunia inakuwa mahali bora na salama pa kuishi

Mitaa ya Jiji la Hamburg Ujerumani, kuzunguka viunga vya Ziwa Alster, zaidi ya watu laki tatu kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamemiminika kuhudhuria mkutano mkubwa ulioandaliwa na Makanisa ya Kiprotestant huko Ujerumani.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo, wamebainisha namna bora ya kuhakikisha kuwa uhasama wa kidini, na baadhi ya viongozi wa serikali kutojali matatizo yanayowakabili wananchi wao vinakomeshwa.

Awali wakiongea na vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali katika ukumbi wa Congres Center Hamburg, Rais wa Makanisa ya Kiprotestanti Ujerumani Profesa Dokta Gerhard Robbers na Katibu Mkuu wake Dokta Ellen Ueberschar, wameelezea nia yao ya kuendeleza mijadala inayogusa maisha ya watu kiroho na kimwili.

Ben Mwaipaja, TBC Hamburg Ujerumani. 

Last Updated ( Friday, 03 May 2013 12:46 )

 

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko China yaongezeka

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko China yaongezeka Idadi ya watu waliokufa nchini China kwa tetemeko la ardhi lililotokea katika Jiimbo la Sichuan imeongezeka kufikia watu 207 majeruhi wakiwa zaidi ya elfu kumi na moja...

Last Updated ( Monday, 22 April 2013 15:20 )

FBI kufanya mahojiano na mtuhumiwa mlipuko Boston

FBI kufanya mahojiano na mtuhumiwa mlipuko Boston Kikosi cha upelelezi nchini Marekani- FBI kinasubiri kufanya mahojiano ya kina na mtuhumiwa wa milipuko iliyotokea mjini humo siku ya jumatatu wakati wa mashindan...

Last Updated ( Monday, 22 April 2013 15:24 )

Kerry awasili Korea Kusini

Kerry awasili Korea Kusini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amewasili Korea Kusini wakati huu ambapo mgogoro baina ya Korea Kaskazini na Korea Kusini unaripotiwa kuendelea. Ker...

Last Updated ( Friday, 12 April 2013 12:44 )

Wagombea urais Venezuela watoa hotuba zao za mwisho

Wagombea urais Venezuela watoa hotuba zao za mwisho Rais wa mpito nchini Venezuela, Nicolas Maduro na mpinzani wake Henrique Capriles wametoa hotuba zao za mwisho kwa wapiga kura wao kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kesh...

Last Updated ( Friday, 12 April 2013 12:41 )

  • «
  •  Start 
  •  Prev 
  •  1 
  •  2 
  •  3 
  •  4 
  •  5 
  •  6 
  •  Next 
  •  End 
  • »
Page 1 of 6
Banner