Home About Tanzania Serikali kuweka umeme mpaka wa Mutukula kwa Bilioni 12

Serikali kuweka umeme mpaka wa Mutukula kwa Bilioni 12

Waziri wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta Serikali imepanga kutumia Shilingi bilioni 12 kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme katika mji wa Mutukula uliopo wilayani Misenyi Mkoani Kagera Mji unaopakana na nchi jirani ya Uganda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afrika ya Mashariki Samwel Sitta alipofanya ziara ya kiserikali kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa Waziri Sitta amesema wamekubaliana na nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki kuwa  hati za wananchi wa maeneo ya mipakani zitolewe na viongozi wa vijiji kwa lengo la kuimarisha mahusiano mazuri miongoni mwao.

Awali akisoma taarifa ya Mkoa  kwa Waziri wa Sitta, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe amesema Mkoa wa Kagera kwa sasa unakabiliwa na wahamiaji haramu elfu 35 ,idadi ambayo  ni hatari kama  hakutakuwa na hatua za makusudi za kuwarejesha makwao.

Pia Waziri Sitta alipata fursa ya kutembelea jengo la ushuru wa pamoja ambalo linajengwa katika eneo hilo la Mutukula, Jengo litakalosaidia kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya ushuru na forodha kwa nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Charles Mwebeya, TBC Kagera.

Last Updated ( Wednesday, 29 August 2012 12:11 )  
Banner