Mkuu wa wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Deodatus Kinawiro amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo na taifa kwa ujumla kuwa
mchakato wa utafiti wa Nishati ya Mafuta kuzunguka Ziwa Rukwa utaanza hivi karibuni na kwamba itakapobainika kuwa kuna mafuta eneo hilo huenda adha ya mafuta nchini ikabaki kuwa ni Historia.
Akifungua kikao cha baraza la Halamshauri ya wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa watafiti hao kwa lengo la kufanikisha zoezi hilo.
Nishati ya mafuta ambayo imekuwa ikilikabili taifa mara kwa mara, taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro mbele ya
madiwani wa wilaya hiyo yaweza ikawa ni suluhisho la uhaba wa nishati ya mafuta nchini.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)