Home About Tanzania Wauza Vitunguu Manispaa ya Singida walalamikia mazingira duni

Wauza Vitunguu Manispaa ya Singida walalamikia mazingira duni

Wafanyabishara na wakulima wa vitunguuWafanyabishara na wakulima wa vitunguu Manispaa ya Singida wameitaka manispaa hiyo kuchukua hatua za haraka za kuwajengea soko la kisasa litakalowawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.

Wamesema soko lililopo hivi sasa ni dogo na halikidhi mahitaji hali ambayo inasababisha kufanyia biashara zao barabarani na kwenye makazi ya watu na kusababisha kero na adha kwa wafanyabiashara hao.

Wamesema kuwa eneo hilo la mauzo limejipatia umaarufu katika Afrika Mashariki na kati kutokana na biashara kubwa ya vitunguu inayofanyika hapo lakini pamoja na umaarufu huo eneo hilo limekuwa kero kwa wafanyabiashara na wakazi wengine.

Wafanyabiashara hao pia wamelalamikia hali ya mazingira ya soko hilo kuwa pia si ya kuvutia ikilinganishwa na biashara kubwa inayofanyika hapo kwani sehemu kubwa imezungukwa na taka taka za vitunguu.

Leonard Manga, TBC Singida

Last Updated ( Tuesday, 22 May 2012 12:12 )  
Banner