Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home About Tanzania Sweden Yaombwa Kuimarisha Viwanda Tanzania

Sweden Yaombwa Kuimarisha Viwanda Tanzania

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Cyril Chami Waziri wa Viwanda na Biashara DKT. CYRIL CHAMI ameiomba serikali ya SWEDEN kuendelea kuisaidia TANZANIA katika utekelezaji wa program ya kuendeleza biashara na kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani ya bidhaa.

Akizungumza na ujumbe wa wawekezaji wa SWEDEN ulioongozwa na waziri wa biashara wa  nchi hiyo EWA HELENA BJORLING  ofisini kwake jijini DSM  DR CHAMI amesema ingawa biashara kati ya nchi hizo imeongezeka kwa asilimia 36, TANZANIA haijanufuika na biashara hiyo kwa sababu haina bidhaa za kutosha za kuuza nchini SWEDEN.

Kwa upande wao wawekezaji wa SWEDEN hapa nchini wameelezea matatizo ya ukosefu wa nishati ya umeme, rushwa na utozaji wa kodi mara mbili unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA kuwa vinakwamisha biashara zao.

Last Updated ( Friday, 27 January 2012 13:56 )  
Banner