Serikali imezungumzia umuhimu wa benki za biashara nchini kutumia mabadiliko ya Teknolojia ya Mawasiliano- TEKNOHAMA-katika kuboresha huduma kwa mteja ikiwa ni pamoja na kuondoa misongamano katika matawi na mashine za kutolea fedha.
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa Mawasiliano, Sanyansi Na Teknolojia CHARLES KITWANGA wakati wa uzinduzi wa huduma ya kifedha ya EAZY PESA ya kampuni ya simu ya Zantel jana usiku jijini DSM ambapo amesema baadhi ya taasisi za fedha zimeshindwa kutumia TEKNOHAMA kuboresha huduma kwa wateja wao.
Naye makamu mwandamizi wa Rais wa kampuni ya ETISALAT ambayo ni kampuni tanzu ya Zantel Ahmed Mokhles amesema huduma ya EZY PESA imefanyiwa marekebisho kutoka huduma ya awali ya Z-Pesa ambapo kwa sasa mteja anaweza kutuma fedha kwa urahisi na kwa haraka zaidi.
