Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home About Tanzania Tanzania kushinda soko la utalii la Marekani

Tanzania kushinda soko la utalii la Marekani

Rais wa Shirikisho la Utalii la Marekani, Lisa SimonRais wa Shirikisho la Utalii la Marekani Lisa Simon amesema Tanzania ni nchi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo inaweza kushinda soko la Utalii la  marekani kwa sasa kutokana na kutokabiliwa na tishio la mashambulizi ya Alshabaab.

Lisa ametoa maelezo hayo wakati akitoa mafunzo kwa wamiliki wa makampuni ya utalii kanda ya kaskazini ambapo amesema wamarekani kwa sasa wanapenda kuhakikishiwa usalama wao pamoja na kupata huduma bora zinazoendana na fedha wanayolipia huduma hizo.

Makampuni ya utalii ya hapa nchini yatafanikiwa ikiwa tu yataboresha huduma hizo pamoja na kuingia mikataba ya kibiashara na makampuni ya utalii ya marekani ambayo yena uzoefu na yenye mtaji wa kutosha.

Katibu wa Chama cha watoa huduma za utalii hapa nchini Mustafa Akunay pamoja na Mwenyekiti wa chama hicho Leopold Kabendera wanaohudhuria mafunzo hayo amesema bodi ya Utalii imeshindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi kwa kushindwa kutangaza vivutio vya utalii ndani ya nchi na nje ya nchi na hivyo kutoa nafasi kwa nchi jirani kutumia vivutio vya hapa nchini.

Last Updated ( Thursday, 19 January 2012 15:47 )  
Banner