Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home You and Your Family Spain Warudi tena Kileleni

Spain Warudi tena Kileleni

Spain Football teamMabingwa wapya wa soka duniani HISPANIA wamerejea tena kileleni kwenye msimamo wa ubora wa shirikisho la kandanda la Kimataifa wakati BRAZIL wakishuka mpaka nafasi ya tatu na ITALY kuporomoka mpaka nafasi ya 11 kutoka nafasi ya TANO.

UHOLANZI walioshindwa kwenye fainali wao wameruka kwa nafasi mbili juu na sasa wanakamata nafasi ya pili ya ubora duniani.

Kwa mshangao wa wengi, ENGLAND ambao walichemsha kwenye fainali hizi wamekwea juu kutoka nafasi ya nane mpaka ya saba.

URUGUAY nao wamepiga hatua kubwa kwa kuruka kwa nafasi KUMI juu na sasa wanakamata nafasi ya SITA, UFARANSA wao wameshuka vibaya, kutoka nafasi ya 12 mpaka ya 21.

UJERUMANI na ARGENTINA wote wamepata, UJERUMANI nafasi nnne na ARGENTINA katika nafasi ya TANO.

NEW ZEALAND,waowamepiga hatua kubwa kwa nafasi 24 na sasa wako katika nafasi ya 54 baada ya kumaliza mechi zake za kombe la dunia bila kufungwa mchezo hata mmoja.

BAFANA BAFANA  wenyeji wa fainali za kombe la dunia wamepanda kwa nafasi 17 na sasa wanakamata nafasi ya 66.

Timu za AFRIKA zilizoko nafasi za juu ni 9. EGYPT (11), 23 GHANA, 26 CÔTE D'IVOIRE, 30 NIGERIA, 33ALGERIA, 34 GABON, 40 CAMEROON.

Last Updated ( Thursday, 15 July 2010 11:32 )  
Banner