Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home You and Your Family Pelegrin atimuliwa,Mourinho achukua nafasi

Pelegrin atimuliwa,Mourinho achukua nafasi

Aliyekua kocha wa Inter Millan,JOSE MOURINHO

Kocha MANUEL PELLEGRIN ametimuliwa kazi katika timu ya REAL MADRID huku kocha JOSE MOURINHO akitangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo.

Rais wa REAL  MADRID  –FLORENTINO PEREZ ametangaza kutimuliwa kibarua kwa PELEGRIN na kuanza rasmi kwa mchakato wa kuwa na MOURINHO siku 5 baada ya kuonekana akiondoka na MOURINHO katika gari lake baada ya fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya  MOURINHO kuonekana akitokwa na machozi wakati akiwaaga wachezaji wake.

Timu ya INTER MILLAN inataka ilipwe EURO millioni 16 kama fidia ya kuvunja mkataba na kocha huyo anayemaliza mkataba wake na INTER mwaka 2012.

Lakini pamoja na yote hayo MOURINHO ndio kocha mpya wa  REAL MADRID ambapo bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo imemtangaza kuwa anakuwa kocha wao huku wakiwa tayari kwa fungu lolote kuwa naye huku mazungumzo yakiendelea na atatambulishwa rasmi muda wowote kuwa ni kocha wa REAL.

Last Updated ( Thursday, 27 May 2010 13:50 )  
Banner