Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home You and Your Family Adebayor aamua kustaafu soka la kimataifa

Adebayor aamua kustaafu soka la kimataifa

Mchezaji wa Manchester City,Emanuel Adebayour

Mchezaji wa kimataifa wa TOGO na klabu ya MANCHESTER CITY, EMMANUEL ADEBAYOR, ameamua kutundika daruga zake katika medani ya kimataifa mapema.

Uamuzu huo wa ADEBAYOR, umekuja ikiwa ni meizi mitatu tangu waasi wa kikundi cha FLEC cha nchini ANGOLA kulivamia basi la wachezaji wa TOGO  wakati wa mashindano ya mataifa ya AFRIKA, mapema mwaka huu, ambapo watu watatu walifariki dunia.

Taarifa ya nyota huyo wa TOGO mwenye umri wa miaka 26 inasema kuwa kufuatia matukio hayo ya kutisha, nimeamua kutoa maamuzi magumu ya kustaafu kucheza soka ya kimataifa.

ADEBAYOR ameongeza kuwa bado anasumbuliwa picha nzima ya tukio hilo alivyolishuhudia siku hiyo mchana.

ADEBAYOR ameichezea timu yake ya taifa kwa muda wa miaka tisa.

Baada ya uvamizi huo wa kikundi cha waasi cha FLEC serikali ya TOGO iliiondoa timu hiyo katika mashindano hayo.

Kutokana na kitendo hicho cha serikali ya TOGO kuiondoa timu hiyo ya taifa, shirikisho la soka barani Afrika CAF, liliifungia nchi hiyo kushiriki mashindano hayo ya mataifa ya Afrika kwa muda wa miaka miwili pamoja na faini ya dola za kimarekani 50,000.

Last Updated ( Wednesday, 14 April 2010 08:26 )  
Banner