
Mcheza gofu nambari moja duniani TIGER WOODS atangumza na wanahabari nusu saa ijayo huko MAREKANI.
WOODS anatarajiwa kuzungumzia kurejea kwake kwenye mashindano makubwa ya gofu ya AGUSTA MASTER kuanzia tarehe nane mwezi huu.
WOODS jana alifanya mazoezi ya wazi akijiandaa na michuano hii, ikiwa ni mashindano yake ya kwanza toka mwezi NOVEMBA mwaka jana alipopata ajali ya gari kwenye eneo la makazi yake baada ya kufarakana na mkewe ELIN kwasababu ya TIGER WOODS kutoka nje ya ndoa na akina dada wapatao 12, jambo ambalo limeharibu sana taswira ya ndoa yake.



