
Serikali za nchi za bara la AFRIKA zimeshahuriwa kubadili mtazamo wa sera zao za kilimo kwa kuwekeza katika kuelimisha wakulima wadogo badala ya kusisitiza uwekezaji wa kilimo cha mashamba makubwa ya wawekezaji wachache.
Kutokana na kasi ya wawekezaji kujilimbikizia sehemu kubwa ya ardhi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kuitumia ardhi hiyo katika shughuli zingine tofauti na kilimo kumepelekea baadhi ya nchi kupoteza mwelekeo wa sera zao
Katika ripoti iliyotolewa na DOKTA LOLENZO COTULA mtafiti wa taasisi ya kimataifa ya mazingira na maendeleo IIED imetahadharisha kuwa usalama wa chakula kwa wakulima wadogo wanaotegemea ardhi upo mashakani kama ilivyojitokeza kwa nchi za TANZANIA na MSUMBIJI ambapo wawekezaji wa nishati mbadala ya BIOFUEL waliopewa mashamba makubwa wameyatumia kinyume na mikataba yao ya uwekezaji .
Msemaji wa taasisi hiyo DAKTA LOLENZO COTULA anashahuri kuwa endapo kunahitajika wawekezaji kutoka nje basi mfumo mzuri ni ule unaowawezesha wakulima wadogo badala ya wakulima wa mashamba makubwa kama ilivyo kwa wakulima wa KAKAO nchini GHANA ambapo wakulima elfu 60 wanamiliki soko kwa miaka 15 na sasa wanamiliki asilimi 45 ya hisa za kiwanda cha CHOKOLETE kilichopo nchini UINGEREZA.