Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Technology Diallo aongoza kwa kura-Guinea

Diallo aongoza kwa kura-Guinea

Waziri Mkuu wa zamani nchini GUINEA CELLOU DALEIN DIALLO

  Waziri Mkuu wa zamani nchini GUINEA CELLOU DALEIN DIALLO pamoja na mwanasiasa mkongwe wa chama cha upinzani nchini humo ALPHA CONDE wanatarajiwa kuchuana katika marudio ya uchaguzi mkuu nchini humo.

 

 Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana usiku na Tume ya Uchaguzi nchini humo wanasiasa hao wanaongoza miongoni mwa wagombea ISHIRINI NA WANNE waliojitokeza kuwania nafasi ya urais ambapo DIALLO amepata Asilimia 39.72 wakati CONDE ana Asilimia 20.67 ya kura. 

Uchaguzi wa awali ulifanyika tarehe ISHIRINI NA SABA mwezi uliopita ambapo matokeo ya uchaguzi huo yametangazwa baada ya kuongezewa siku mbili na Mahakama ya Rufaa ili kuiwezesha Tume ya Uchaguzi kuhesabu kura.

Uchaguzi huo ni wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika nchini  GUINEA  tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa UFARANSA mwaka 1958.Watu waliojitokeza katika uchaguzi huo ni watu Milioni TATU Nukta TATU miongoni mwa watu Milioni NNE Nukta MBILI waliojiandikisha.

 

 

   

 
Banner