
Mgombea wa chama chenye ushindani mkubwa na rais Omar Bashiri wa Sudan amejitoa katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya uraisi ikiwa zimebaki siku chache tu kuanza kufanyika kwa uchaguzi nchini humo.
chama hicho cha sudan people’s liberation movement SPLM kimesema Yassir Aramn hatagombea nafasi hiyo ya urais dhidi ya rais bashiri kutokana na kuhofia kuzuka kwa mapigano pamoja na kile walichodai kutokuwa na imani na mfumo mzima wa uchaguzi huo ambao ni wa kwanza kufanyika tangu mwaka 1986.
Uchaguzi wa serikali za mitaa na majimbo unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 mwezi huu huku kukiwa kumetanda hali ya wasiwasi ya kuzuka kwa mapigano mapya