Kiongozi wa majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya KONGO –DRC, Alan Doss amesema mikakati mipya inahitajika kwa ajili ya kuzuia mauaji ya watu wengi yanayofanywa na kikundi cha waasi cha LORD’S RESISTANCE ARMY –LRA.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa mauaji ya zaidi ya watu mia tatu, kaskazini mashariki mwa DRC, Kiongozi huyo amesema ndege za doria kwa ajili ya kuimarisha usalama, zinahitajika pamoja na kuwepo kwa uchunguzi makini.
Hata hivyo Alan Doss amesema, kutokana na kundi



