Mgombea wa Ubunge mkoani TANGA afariki dunia
Mgombea Ubunge wilayani LUSHOTO mkoani TANGA kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA MOHAMED MTOI KANYAWANA amefariki dunia kwa ajali ya Gari
MOHAMED MTOI KANYAWANA

Mgombea Ubunge  wilayani LUSHOTO mkoani TANGA  kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA MOHAMED MTOI KANYAWANA amefariki dunia kwa ajali ya Gari iliyotokea katika kijiji cha MAGAMBA  wilayani HANDENI mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini DSM Mkuu wa idara ya habari  na mawasiliano CHADEMA, TUMAINI MAKENE amesema ajali hiyo imetokea wakati marehemu MTOI akirudi nyumbani kwake kutokea  kwenye mkutano wa kampeni  jimboni kwake.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo SAA SABA mchana huko kijijini kwao MKUZI, LUSHOTO  mkoani TANGA.

Marehemu ameacha mke na watoto wawili

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI