KINANA: Dkt MAGUFULI kuunda baraza dogo la mawaziri
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - ABDULRAHMAN KINANA amesema endapo Dkt. JOHN MAGUFULI atachaguliwa kuwa Rais atapunguza ukubwa
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - ABDULRAHMAN KINANA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi - ABDULRAHMAN KINANA amesema endapo Dkt. JOHN MAGUFULI atachaguliwa kuwa Rais atapunguza ukubwa wa serikali kwa kuunda baraza dogo la mawaziri.

 

Akizungumza katika mikutano ya kampeni ya kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. JOHN MAGUFULI mkoani MBEYA, KINANA amesema  lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuelekeza fedha kwenye uboreshaji wa huduma za afya, kilimo na kulipa madeni ya waalimu.

 

Amesema pamoja na kupunguza ukubwa wa serikali pia ataunda baraza dogo la mawaziri wawajibikaji na wazalendo ambao wataweza kusimamia ufanisi serikalini.

 

Amewataka wakazi wa wilaya za MBOZI na TUNDUMA kumchagua Dkt. MAGUFULI ili aharakishe ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji na kuboresha huduma za afya.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI