Zaidi ya Mahujaji 100 wafariki dunia baada ya kuangukiwa na winchi katika msikiti mkuu wa MAKKA, SAUDI ARABIA
Zaidi ya Mahujaji 107 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 230 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na winchi katika Msikiti Mkuu wa MAKKA, SAUDI ARABIA
Zaidi ya Mahujaji 100 wafariki dunia baada ya kuangukiwa na winchi katika msikiti mkuu wa MAKKA, SAUDI ARABIA

Zaidi ya Mahujaji 107 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 230 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na winchi katika Msikiti Mkuu wa MAKKA, SAUDI ARABIA.

Habari zinasema winchi hiyo kubwa imeangukia katika Msikiti huo mkubwa duniani ambao kwa wakati huo ulikuwa umejaa waumini katika Swala ya Ijumaa.

Mkuu wa Idara ya Ulinzi huko SAUDI ARABIA amesema upepo mkali na mvua imesababisha kuanguka kwa winchi hiyo.

Kwa wakati huu Mji wa MAKKA unajiandaa kwa ajili ya Ibada ya HIJJA ambapo maelfu ya watu baadae mwezi huu wanatarajiwa kuwasili katika mji huo kutoka kutoka sehemu mbalimbali duniani.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI