Mkuu wa Majeshi wa BURUNDI anusurika kufa
Mkuu wa majeshi wa BURUNDI, Jenerali PRIME NIYONGABO, amenusurika kuuwawa baada ya msafara wake kushambuliwa katika mji mkuu, BUJUMBURA
Mkuu wa Majeshi wa BURUNDI anusurika kufa

Mkuu wa majeshi wa BURUNDI, Jenerali PRIME NIYONGABO, amenusurika kuuwawa baada ya msafara wake kushambuliwa katika mji mkuu, BUJUMBURA.   

Naibu mkuu wa polisi, Jenerali GODEFROID BIZIMANA amesema watu SABA wameuawa kwenye mashambulizi hayo wakiwemo washambuliaji WAWILI ambapo mmoja wao amekamatwa.

Afisa mwingine wa polisi amesema walinzi WANNE wa Jenerali huyo pamoja na afisa mmoja wa polisi mwanamke wameuwawa.

Mashuhuda wanasema washambuliaji walikuwa wamevalia sare za kijeshi na walikuwa kwenye gari la kijeshi.

Polisi wamesema inawatafuta washambuliaji wengine, ambao wanatuhumiwa kuwa wa kikosi cha makamando

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI