Bondia THOMAS MASHALI atamba kumpiga mpinzani wake FRANCIS CHEKA
Bondia THOMAS MASHALI ametamba kumpiga mpinzani wake bondia FRANCIS CHEKA katika pambano lililopangwa kufanyika mkoani MOROGORO Desembar 25 mwaka huu
Bondia THOMAS MASHALI

Bondia THOMAS MASHALI ametamba kumpiga mpinzani wake bondia FRANCIS CHEKA katika pambano lililopangwa kufanyika mkoani MOROGORO Desembar 25 mwaka huu.

Akizungumza jijini DAR ES SALAAM, MASHALI amesema hakuna bondia anayemsumbua hapa nchini na hamuogopi FRANCIS CHEKA.

Amesema yuko katika maandalizi ya kutosha yakianzia hapa DAR ES SALAAM kisha kwenda visiwani ZANZIBAR kwa ajili ya kambi.

Bondia THOMAS MASHALI anashikilia ubingwa wa AFRIKA alioutetea baada ya kumpiga bondia IBRAHIM TAMBA mwezi Septemba mwaka huu

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI