Uchaguzi mkuu nchini GUINEA kufanyika kesho Jumapili
Rais ALPHA CONDE wa GUINEA amesema uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika keshokutwa Jumapili kama ilivyopangwa na kutupilia mbali wito uliotolewa
Rais ALPHA CONDE wa GUINEA

Rais ALPHA CONDE wa GUINEA amesema uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika kesho Jumapili kama ilivyopangwa na kutupilia mbali wito uliotolewa na upinzani kutaka kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Kiongozi wa upinzani, CELLOU DALEIN DIALLO ameomba kuahirishwa kwa uchaguzi wa Rais nchini humo ili kutoa fursa kwa waangalizi wa kimataifa kuchunguza madai ya wizi wa kura na kuandikishwa kwa watu wenye umri mdogo kuliko ule unaoruhusiwa kupiga kura.

Mapigano yameripotiwa kutokea katika mji mkuu wa GUINEA, CONAKRY ikiwa ni siku chache kabla ya siku ya kupiga kura

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI