Kiongozi wa mapinduzi nchini BURKINA FASO ashtakiwa
Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini BURKINA FASO mwezi uliopita ameshtakiwa kwa makosa 11 ikiwemo kutishia usalama wa taifa hilo na mauaji
Jenerali GILBERT DIENDERE

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini BURKINA FASO mwezi uliopita ameshtakiwa kwa makosa 11 ikiwemo kutishia usalama wa taifa hilo na mauaji.

Jenerali GILBERT DIENDERE anatarajiwa kujibu mashtaka hayo katika mahakama ya kijeshi.

Rais wa mpito MICHEL KAFANDO alirejeshwa madarakani wiki mbili zilizopita baada ya jeshi la nchi hiyo na viongozi wa nchi za AFRIKA Magharibi kuingia kati mgogoro nchini BURKINA FASO.

Kikosi cha ulinzi cha Rais kilichofanya mapinduzi ya kijeshi kinatarajiwa kufumuliwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani nchini BURKINA FASO, DJIBRIL BASSOLE, ambaye pia alikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mapinduzi hayo pia amefunguliwa mashtaka ingawaje amekanusha kuhusika na mapinduzi hayo.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI