Wanaojihusisha na pombe aina ya CHANG’AA wachapwa viboko
Wakazi wa eneo la CHANYA katika kaunti ya KIAMBUU nchini KENYA wamewacharaza viboko wanywaji na wauzaji na wapika pombe haramu ya gongo nchini humo
Utengenezaji wa pombe ya Chang'aa

Wakazi wa eneo la CHANYA katika kaunti ya KIAMBUU nchini KENYA wamewacharaza viboko wanywaji na wauzaji na wapika pombe haramu ya gongo nchini humo, maarufu kama CHANG’AA, baada ya kubaini maficho yao.

Watu hao walivamia maficho ya mapishi ya gongo, katika eneo moja la pembezoni.

Watu hao wanasema wameamua kuwachapa wapika gongo, wanywaji na wauzaji kwa vile wamekiuka amri ya rais UHURU KENYATTA wan chi hiyo ya kukataza unywaji na upishi wa pombe haramu.

 

Zaidi ya watu kumi na watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na upishi, pamoja na ufanyaji biashara haramu ya CHANG’AA.

 

Wananchi wa KENYA mara kadhaa wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi dhidi ya wafanyabiashara wa chang’aa kwa madai kuwa pombe hiyo inaathiri maisha ya watu wengi katika familia.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI