YAMOTO BAND kukabidhiwa nyumba za kuishi
Mmiliki wa kituo cha muziki cha MKUBWA na WANAWE SAID FELLA amesema anatarajia mwaka huu Rais wa awamu ya NNE JAKAYA KIKWETE atazindua nyumba nne za wanamuziki wa YAMOTO BAND zilizopo jijini DSM.
Mmiliki wa kituo cha muziki cha MKUBWA na WANAWE SAID FELLA

Mmiliki wa kituo cha muziki cha MKUBWA na WANAWE SAID FELLA amesema anatarajia mwaka huu Rais wa awamu ya NNE JAKAYA KIKWETE atazindua nyumba nne za wanamuziki wa YAMOTO BAND zilizopo jijini DSM.

FELLA amesema kutokana na mchango mkubwa aliyoupata kwa Rais huyo wa awamu ya nne ameona ni vyema akampatia fursa ya kuzizindua nyumba hizo zilizopo nje CHAMAZI nje kidogo ya jiji la DSM.

Aidha FELLA ameongeza kuwa matarajio yao kwa mwaka 2016-17 ni kupanua zaidi kituo na kutoa nyimbo zaidi huku akisema kwa sasa ameamua kusitisha kuchukua vijana kwenye kituo hicho kutokana na kuwa wengi kiasi cha kumzidi uwezo wa kuwahudumia.

Vilevile SAID FELLA amesema wanafurahi kumkaribisha KAYUMBA mshindi wa BSS ambaye alikua kwenye kikundi hicho kabla ya kuruhusiwa kwenda kushiriki shindano hilo.

Vijana waliopo kwenye kituo hicho mpaka sasa ni 102 ambao wanaimba muziki wa miondoko mbalimbali. Tupane kuona vionjo kidogo.

March 4, 2016

Na OSCAR URASSA

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI