Mafuriko nchini JAPAN, watu 2 hawajulikani walipo
Watu wawili hajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa kuikumba nchi ya JAPAN kwa siku kadhaa
Mafuriko nchini JAPAN, watu 2 hawajulikani walipo

Watu wawili hajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa kuikumba nchi ya JAPAN kwa siku kadhaa.

Watu wengi wamekwama katika maeneo mbalimbali baada ya kingo za mito mikubwa iliyoko kaskazini mwa mji wa TOKYO nchini humo kupasuka.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la JAPAN mvua yenye ujazo wa milimita zaidi ya 500 zimenyesha katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Idara ya hali ya hewa imetabiri kuwa nchi hiyo itaendelea kukabiliwa na mvua kubwa, zinazoambatana na mafuriko.

Nchi hiyo hukabiliwa na mvua za msimu katika mwezi Septemba. Waziri mkuu wa JAPAN SHINZO ABE amesema serikali yake itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa raia wake wanakuwa salama, na kuandaa maeneo ya dharura ya misaada kwa ajili ya uokozi.

Baadhi ya watu wameendelea kubaki juu ya mapaa ya nyumba zao, huku maeneo mengine yakikabiliwa na maporomoko ya udongo. Miongoni mwa watu wasiojulikana mahali walipo ni Mwanamke mmoja ambaye nyumba aliyokuwa akiishi ilibomoka na kuporomoka kwenye maji.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI